CRDB Bank Federation Cup

CRDB Bank Federation Cup kwa sasa ni hatua ya robo fainali ambapo kila timu imetambua ilipogotea baada ya dakika 90 kwenye msako wa ushindi katika hatua ya 16 bora.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ambao ni Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi wamepenya katika hatua ya 16 bora wakipata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji.

Leo saa 6:00 Aprili 17 droo ya robo fainali itafanyika na kuruka mubashara kupitia AzamSports3HD.

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ni Namungo FC, Geita Gold FC, Tabora United, Coastal Union, Ihefu SC, Azam  FC, Mashujaa FC na Yanga.

Hivyo kila timu inakwenda kutambua itakutana na nani kwenye hatua ya robo fainali kusaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here