BAADA ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC, mabosi wa Simba wamekuja na mpango kazi kwa ajili ya mechi znazofuata.

Ipo wazi kuwa Februari 9 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Simba 1-1 Azam FC.

Prince Dube alipachika bao dakika ya 14 huku Clatous Chama akifunga bao la kuweka usawa dakika ya 90.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema:”Tunamshukuru Mungu kwa matokeo tuliyopata, Si mazuri sana na si mabaya sana

“Tunawapongeza wachezaji wetu kwa kupambana na kuvuna alama moja kwani bila upambanaji wao tusingeipata

“Hili limekwisha, Sasa tunaangalia zaidi mechi ijayo. Asanteni Mwanza, Asante kanda ya Ziwa, Asanteni wana Simba. Jicho letu sasa ni Feb 12 dhidi ya Geita Gold hapa hapa Kirumba,”.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 30 Azam FC nafasi ya pili na pointi 32.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here