KITAIFA

MKALI WA MABAO KAMILI SIMBA KUWAKABILI JKT TANZANIA

JEAN Ahoua kiungo mshambuliaji namba moja kuhusika katika mabao ndani ya kikosi cha Simba SC, mabao 12 na pasi 7 za mabao akiwa ni mkali wa mabao ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Kahusika katika jumla ya mabao 19 kati ya 54 yaliyofungwa na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 60 kibindoni baada ya mechi 23.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa FC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex Mei 2 2025 na baada ya dakika 90 ubao kusoma Simba 2-1 Mashujaa FC, Ahoua hakuwa sehemu ya mchezo.

Sababu iliyomfanya awe nje ni maumivu ya misuli ambayo alipata kwenye mechi za kimataifa hatua ya nusu fainaliI Kombe la Shirikisho Afrika ila kwa sasa ameendelea kutengamaa.

Mei 5 2025 ni JKT Tanzania vs Simba mzunguko wa pili, Uwanja wa Isamuhyo saa 10:00 jioni kwenye mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba 1-0 JKT Tanzania bao likifungwa na Ahoua kwa mkwaju wa penati dakika ya 90.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button