NYOTA wa Yanga SC Pacome Zouzoua inaelezwa kuwa ameitwa na mabosi wa timu hiyo ili kujadili kuhusu kuongeza mkataba kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Pacome ni chaguo la kwanza la Hamdi ambapo kwenye msimu wa 2024/25 kacheza jumla ya mechi 23 Pacome kahusika kwenye mabao 18 akiwa kafunga mabao 9 na kutoa pasi 9 za mabao msimu wa 2024/25.
Ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kasepa na dakika 1,364 ndani ya uwanja kwenye mechi 23 ambazo alipata kucheza kati ya 26.
Nyota huyo kakosekana kweye mechi tatu pekee ambazo ni dakika 270 na zote hizo ilitokana na kutokuwa fiti na miongoni mwa mchezo ambao umemfanya awe nje kwa muda ni Dar Dabi dhidi ya Azam FC alipopata maumivu kipindi cha kwanza.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga SC wapo kwenye mazungumzo na Pacome ili kumuongezea mkataba mpya abaki ndani ya kikosi hicho kuendelea kutimiza majukumu yake.