Klabu ya Mashujaa Fc imekwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara kufuatia sare ya tasa dhidi ya Wajelajela, Tanzania Prisons katika dimba la Lake Tanganyika, Kigoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.
Baada ya timu hizo kugawana alama Mashujaa imefikisha pointi 4 baada ya mechi mbili na kuiporomosha Simba Sc mpaka nafasi ya pili.
Hii ni sare ya pili mfululizo kwa Tanzania Prisons ambayo ipo nafasi ya nne pointi 2 baada ya mechi mbili .
FT: Mashujaa FC 0-0 Tanzania Prisons