Kocha wa timu ya Taifa Uholanzi Ronald Koeman amesema wazi kuwa ameacha kumuita mchezaji wake nyota wa timu ya taifa ya Uholanzi Steven Bergwijn kwasababu ameondoka kwenye ligi ya Uholanzi na kujiunga na klabu ya Al Ittihad ya ligi ya Saudia.
“Kama una miaka 26 kitu muhimu zaidi n kucheza siyo pesa. angebaki tu Ajax wanalipa vizuri pia, kwa umri wake hakupaswa kufanya uamuzi kama ule. nimefunga mlango wake wa kuichezea timu ya Taifa ya Uholanzi” alisema Koeman.
Steven Bergwijn mwenye umri wa miaka 26 hadi sasa ameichezea Uholanzi michezo 35 akiwa na magoli 8.