yanga usajili

Viongozi wa Yanga SC wamepambana kwelikweli kuhakikisha wanaboresha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao na wanashusha vyuma kwelikweli.

Za ndani kabisa zinaeleza tayari wamemalizana na mshambuliaji Prince Dube raia wa Zimbabwe ambae bado yupo kwenye mgogoro na klabu yake ya Azam FC ni moja ya washambuliaji Bora sana kwenye Ligi yetu.

Kuna jina la Jonathan Sowah kutokea kule nchini Ghana amemaliza mkataba na klabu ya Al Nassr ya Libya nae inaelezwa tayari amemalizana na viongozi wa Yanga SC watu wengi wanafahamu namna Bakari Nondo Mwamnyeto alivyolambishwa nyasi.

George Mpole amewahi kuwa mfungaji bora wa NBC Premier League msimu wa 2021-22 mbele ya Fiston Kalala Mayele akitimkia zake Saint Eloi Lupopo inaelezwa kuwa Yanga SC wapo mbioni kumrejesha nyota huyo.

Nyota hawa wote wanatajwa kuelekea Jangwani kurekebisha eneo ambalo limeonekana toka Mayele ajiunge Pyramids.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here