Yanga

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa mipango yao ipo palepale kupambana kufikia malengo ya kutwaa ubingwa kwa kuwa hilo ni jambo ambalo walianza nalo kazi mapema mwanzo wa msimu.

Chini ya Miguel Gamondi, Yanga imekuwa ikipata matokeo kwenye mechi zake za ushindani huku safu ya ushambuliaji ikiwa inaongozwa na kiungo mshambuliaji Aziz KI mwenye mabao 15 akiwa namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi.

Yanga mchezo wake uliopita baada ya dakika 90 ikiwa ugenini ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Meja Isamuhyo ukisoma JKT Tanzania 0-0 Yanga hivyo waligawana pointi mojamoja.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga aliweka wazi kuwa bado kazi haijaisha kwa kuwa kuna mechi ambazo watacheza watapambana kufanya vizuri kufikia malengo ya kutetea taji la ligi.

“Kuna ushindani mkubwa kwenye mechi ambazo tunacheza hilo tunalitambua kikubwa ambacho tunakifanya ni maandalizi mazuri na wachezaji wanatambua kwamba ili kufikia malengo ni muhimu kupata pointi tatu.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza kwa kuwa kikubwa ni kuona tunapata matokeo na kufikia malengo yetu,”.

Kwenye msimamo wa ligi Yanga ni namba moja wakiwa na pointi 59 baada ya kucheza mechi 23msimu wa 2023/24.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here