Kiungo wa kati wa klabu ya Chelsea na timu ya Taifa ya Uingereza Conor Gallagher yupo mbioni kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Atletico Madrid ya Uhispania kwa mkataba wa miaka mitano na ada ya usajili ya Paundi Milioni 40 (zaidi ya Tsh bilioni 138).
Gallagher ambaye alishiriki michuano ya kombela Mataifa ya Ulaya (EURO 2024) ana uwezekano mkubwa kujiunga na Atletico kwasababu siyo mmoja wa wachezaji wanaotajwa kuhitajika zaidi na kocha mpya Enzo Maresca.