Chombo cha Habari cha Lusaka Times, kimeeleza kuwa gari iliyopata ajali ikiwa na nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia na klabu ya TP Mazembe, Rainford Kalaba ilikuwa ikiendeshwa na Charlene Mukandawire mke wa rafiki yake Kalaba aitwaye Boyd Mukandawire.
Mwadada huyo alipoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Aprili 13, 2024 huko Kafue Zambia huku Kalaba akiwa maututi chini ya Uangalizi wa madakitari Bingwa.
Taarifa zinaeleza kuwa Charlene Mukandawire alimuaga mumewe, Boyd Mukandawire kwamba anaenda kumsalimia rafiki yake huko Kafue kisha baadaye taarifa zikatoka amefariki katika ajali akiwa kwenye Gari ya Rainford Kalaba.