Nyota wa Inter Miami na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ametoa maoni yake baada ya aliyekuwa nyota mwenzake wa Barcelona Andres Iniesta kutangaza kustaafu soka huku akisema wazi kuwa soka litamkumbuka sana.
Messi ameandika kupitia Insta Story yake;
“Andrés, umekuwa mmoja wa wachezaji wenzangu walio na uchawi mwingi … mmoja wa wale ambao nilifurahia kucheza nao zaidi”.
“Mpira utaku-miss sana, na sisi sote pia.”
“Nakutakia kila la kheri”.