Mama mzazi wa nahodha wa Ureno na Al Nassr Cristiano Ronaldo, Dolores Aviero amemsihi nyota huyo kuendelea kucheza asistaafu mapema hadi pale atakapocheza timu moja na mjukuu wake, (mtoto wa Ronaldo) Cristiano Junior.
“Mama na mwanangu wamekuwa wakinishinikiza kuwa niendelee kwa muda zaidi kucheza ili siku moja nicheze na Cristiano Jr timu moja, najua ni ngumu lakini nitajitahidi kwa miaka mingine zaidi ili tuone inakuwaje” alisema Ronaldo.
Cristiano Jr ambaye kwasasa ana umri wa miaka 14 anacheza timu ya vijana na Al Nassr na anatamani simu moja kucheza timu moja na Ronaldo.