tetesi za soka ulaya

Manchester United wako tayari kumwachia mlinzi wa zamani wa Ufaransa Raphael Varane, 31, kuondoka bure mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (Mirror)

Barcelona wanatazamia kuimarisha safu yao ya mashambulizi huku mshambuliaji wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 27, akiwa mmoja wa walengwa wao wakati The Reds “wakiishiwa na subira” na uchezaji wake. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)

Beki wa Cameroon Joel Matip, 32, ni mchezaji mwingine ambaye anaweza kuondoka Liverpool msimu huu wa joto huku Roma na Lazio zikimwania. (Corriere – kwa Kiitaliano)

Manchester United inatarajia wachezaji kadhaa kuondoka majira ya joto ili kukidhi mahitaji ya usawa wa kifedha michezoni, huku mustakabali wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 26, ukizingatiwa. (Express)

AC Milan wanavutiwa na beki wa Aston Villa Mbrazil Diego Carlos, 31, baada ya kufanya vyema aliporejea kutoka kwa jeraha la Achilles. (Sport – via TeamTalk)

Beki wa Fulham Tosin Adarabioyo, 26, ameiambia klabu hiyo kuwa anakusudia kuondoka kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto, huku Liverpool, Tottenham na Newcastle zikivutiwa na Muingereza huyo. (Express)

Winga wa Brighton na Japan Kaoru Mitoma, 26, ananyatiwa na klabu za Arsenal, Manchester City na Manchester United. (Fichajes – via 90 min)

Paris St-Germain wanakabiliwa na kizingiti katika jaribio lao la kumsajili kinda wa Barcelona na Uhispania Lamine Yamal, 16, huku wakala wa kinda huyo akiiambia klabu hiyo hauzwi. (AS – kwa Kihispania)

Klabu za Arsenal na Tottenham Hotspur zinatazamia kumsajili kiungo wa West Ham aliyewahi kuchezea timu ya Uingereza ya wachezaji wa chini ya miaka 16 Daniel Rigge, 18. (ESPN)

Bayern Munich wamethibitisha kuwa wanafanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Manchester United Ralf Rangnick kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel kama mkufunzi. (Goal)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte amefikia makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya meneja wa Napoli. (Rai kwa Kiitaliano)

Real Madrid hawana mpango wa kumnunua mlinzi wa Bayern Munich Alphonso Davies, 23, msimu huu wa joto lakini wana nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada bila malipo kandarasi yake itakapokamilika 2025. (Relevo – kwa Kihispania).

Arsenal wameanza mazungumzo ya kumpa mkataba mpya beki wa Brazil Gabriel Magalhaes, 26, baada ya kuwa na msimu wa mchezo mzuri. (Mirror)

Beki wa Barcelona Pau Cubarsi, 17, amepewa mkataba wa miaka mitano ambao anatarajiwa kutia saini atakapofikisha umri wa miaka 18 mwezi Januari, licha ya kutakiwa na Manchester City. (AS – kwa Kihispania)

Bologna bado wana matumaini ya kuongeza mkataba wa kocha Thiago Motta baada ya Juni 2024 licha ya Juventus na Manchester United kumtaka Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 41. (Gazzetta dello Sport, kupitia Football Italia)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here