Timu ya matibabu ya Klabu ya Liverpool imethibitisha kuwa kipa namba moja wa klabu hiyo Alisson Berker ameumia nyama za paja na atakuwa nje ya uwanja hadi mwezi Novemba.
Katika kipindi atakachokuwa nje ya uwanja, kipa huyo raia wa Brazi atakosa mechi dhidi ya Chelsea, Arsenal, Brighton, and Aston Villa kwenye ligi kuu Uingereza Premier League, na mbili za Champions League ambazo ni dhidi ya RB Leipzig na Bayer Leverkusen.