MAYELE, INONGA WANARUDI TANZANIA

Wale msiowapenda wanakuja tena, Fiston Kalala Mayele na Henock Inonga Baka, wote kwa pamoja wapo mbioni kurejea Tanzania kwa mara nyingune tena

Mayele na Inonga, watarejea nchini wakiwa na Kikosi cha Timu ya Taifa ya Dr Congo ambacho kimepangwa kundi moja na Tanzania katika kuwania nafasi ya kufuzu michuano ijayo ya Afcon ya mwaka 2025

Kundi H linaundwa na Timu za Tanzania, Ethiopia, Dr Congo na Guinea

Itakumbukwa kuwa Inonga alishawahi kucheza Tanzania akiwa na klabu ya Simba Sc kabla ya kutimkia kunako Klabu ya Far Rabbat ya Morocco na Mayele ambaye alishawahi kuitumikia Yanga Sc kabla ya kusajiliwa na Pyramids ya Misri.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here