Simba

BAADA ya Wagosi wa Kaya Coastal Union kukanusha habari za mchezaji wao Lameck Lawi kusajiliwa na Simba SC, wakisem kwamba hawatambui mkataba wa Simba na Lawi, Crescentius Magori ametolea ufafanuzi wa suala hilo.

Magori amezungumzia suala hilo kwa undani wake huku akisema kwamba, ni kweli walilipa pesa nusu lakini baadae walimalizia zilizobaki.

Magori aliyasema hayo kupitia Chombo cha Habari cha EFM, na kubainisha kwamba, walikubaliana kabla ya chezaji huyo kusajiliwa SIMBA waliwataka Coastal Union wamruhusu kwanza mchezjai huuyo afanyiwe vipimo vya afya.

“Katika hali ya kawaida hatukutegemea hili litokee, kwakuwa limetokea itabidi tukabiliane nalo, lakini mchezaji huyo amesajiliwa na Simba SC na kila kitu kipo tayari”

“Hata hiyo klabu inayomtaka Coastal Union (ya Nje), waambie hatutaishitaki Coastal Unin pekee tutawashitaki wote”

Magori aliendelea kwa kusema haya;

“Ndio tulichelewa kumaliza kulipa pesa, tulilipa nusu lakini mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yoye ya usajili”

“Tumemsajili Lameck Lawi kwa kufuata utaratibu tunafanya kazi kwa uweledi, hoja zao ni dhaifu kusema mkataba umevunjika kwa sababu pesa haikulipwa yote”

“Wangesema mapema kama ukichelewa kulipa mkataba unavunjika. Mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yote na nyaraka zote tunazo hata tukienda FIFA. Mpira ni FIFA hauishii hapa”

“Kilichotokea Coastal Union wakapata deal kutoka nje ndio maana wakabadili maamuz. Kiukweli hili limetusumbua sana na tuko tayari kukabiliana nalo”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here