CHUMA cha kazi ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Prince Dube kimeanza kazi kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ipo wazi kwamba Julai 8 2024 Dube ambaye ni muuaji anayetabasamu alikuwa na uzi wa kijani na njano na kuanza mazoezi kwenye changamoto yake mpya.
2023/24 alikuwa ndani ya Azam FC kabla msimu haujagota mwisho aliomba kuvunja mkataba na mabosi hao wanaotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za nyumbani.
Dube amesaini dili la miaka miwili alifunga jumla ya mabao 7 msimu wa 2023/24 alipokuwa ndani ya Azam FC kabla ya kuamua kuvunja mkataba wake.
Mabingwa watetezi wa ligi Yanga wameshaingia kambini tayari kwa maandalizi kuelekea msimu wa 2024/25.
AlI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wachezaji waliopo ndani ya kikosi hicho ni bora wanawapa nguvu ya kufanya vizuri zaidi.
“Tulifanya kazi nzuri msimu uliopita na tulikuwa na kikosi bora hivyo msimu ujao tunaamini tutakuwa bora zaidi na wachezaji watakuwa ni imara zaidi.”