Hersi Said Yanga

RAIS wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika, Injinia Hersi Said amebainisha kuwa timu ya Yanga inagusa maisha ya kila Mtanzania.

“February 11, mwaka huu, Yanga ilitimiza miaka 89 tangu kuanzishwa kwake. Ni Klabu kongwe zaidi ya mpira wa miguu Tanzania na ilishiriki kwenye harakati za Uhuru wa Taifa letu. Ni timu ya Wananchi inayogusa maisha ya kila Mtanzania anayependa mpira.

“Young Africans SC ni Klabu yenye mafanikio zaidi Tanzania. Ni Mabingwa mara 29 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, anayefatia amebeba Ubingwa mara 22. Msimu huu mpaka sasa tunaongoza Ligi na In Shaa Allah tutapambana kuongeza Taji la 30 kwenye Kabati letu la Makombe,”.

Haya yote amezungumza na Chama cha Waandishi wa Habari za Soka Afrika Kusini, (South African Football Journalist Association -SAFJA).

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here