BAADA ya kukamilisha kazi ya dakika 180 kwenye msako wa Kombe la Muungano, mabingwa wapya ambao ni Simba wamewasili Dar.
Kombe la Muungano 2024 lilifanyika Visiwani Zanzibar lilianzia hatua ya nusu fainali ambapo timu nne zilishiriki kwenye mashindano hayo.
Ilikuwa nusu fainali ya kwanza KVZ 0-2 Simba mabao ya Michael Fred na Israel Mwenda kwa mkwaju wa penalti na nusu fainali ya pili ilikuwa Azam FC 5-2 KMKM.
Hivyo fainali ambayo ilikuwa ni Aprili 27 2024 ubao ulisoma Azam FC 0-1 Simba bao la ushindi likifungwa na Babacarr Sarri.
Leo mapema msafara wa Simba ukiwa na taji hilo ulianza safari kutoka Zanzibar na umewasili salama Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.