KUELEKEA mchezo wa CRDB Federation Cup raundi ya nne kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Yanga, mabingwa watetezi wa taji hilo wameonekana kuwahofia wapinzani wao kutokana na uimara wao.
Pengine ni mtego kwa Dodoma Jiji kwa kuwa Yanga wakiwa na jambo lao huwa hawana hofu zaidi ya kucheza kwa umakini kutafuta ushindi.
Aboutwalib Mshery kipa wa Yanga ameweka wazi kuwa mchezo wao dhidi ya Dodoma jiji hautakuwa mwepesi kwa kuwa wapinzani wao wapo imara.
“Utakuwa mchezo mgumu tunatambua hilo kwani Dodoma Jiji ni timu ambayo imekuwa ikitupa ushindani tunapokutana nao licha ya kwamba tumekuwa tukipata matokeo mbele yao.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo tuaamini haitakuwa kazi nyepesi hivyo tunaamini kwa ushirikiano kutoka kwa wachezaji pamoja na malekezo ya benchi la ufundi tutafanya vizuri,”.
Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wa taji la CRDB Federation ikiwa watashinda kwenye raundi ya nne watatinga hatua ya robo fainali..