WILLY Onana kiungo mshambuliaji wa Simba amesema wapo tayari kuandika historia kwa kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ipo wazi kwamba miongoni mwa waliotimiza majukumu yake katika hatua za makundi ni Onana licha ya kutokuwa na mwendelezo mzuri, mabao yake mawili kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablanca yaliongeza nguvu kwa Simba kutinga hatua ya robo fainali.
Simba imeweka kambi Zanzibar ina kazi ya kufanya dhidi ya Al Ahly, Machi 29 Uwanja wa Mkapa mchezo wa hatua ya robo fainali na kete ya pili itakayoamua mshindi atakayekwenda hatua ya nusu fainali itakuwa nchini Misri.
Onana amesema: “Nipo tayari kwa ajili ya kuandika historia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika natambua kwamba tunapambana na timu bora kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo na kusonga mbele,”.