wachezaji Simba

KWA upande wa wachezaji wa Simba viwango vyao kwa sasa ni maji kupwa maji kujaa, mchezaji anaweza kucheza mchezo wa leo vizuri kesho akawa katika kiwango cha chini.

Miongoni mwa wachezaji hao ndani ya Simba ni Willy Onana, ukimtazama aliyecheza mchezo dhidi ya Namungo kisha ukamuona aliyecheza dhidi ya Mtibwa Sugar tofauti kabisa.

Hii ni hali inayowatesa wachezaji wengi wa Simba na benchi la ufundi, mbele ya Mtibwa Sugar nafasi tano za wazi ndani ya 18 alikosa utulivu na maamuzi mazuri katika kuzitumia nafasi.

Ikumbukwe kwamba mwamba Michael Fred mwenye mabao matano ndani ya Ligi Kuu Bara naye anapita kwenye kipindi hiki.

Mchezo wake dhidi ya Mashujaa akitokea benchi alifanya kazi kubwa na kufunga bao moja hatua ya 16 bora alipopata nafasi mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Liti alikwama kufunga katika mchezo huo.

Katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Fred alifunga bao moja wakati Simba ikishinda mabao 2-0 ikikomba pointi tatu mazima kwenye mchezo huo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here