HII HAPA REKODI RAUNDI YA 8 SI MCHEZO
REKODI zinazidi kuandikwa kila leo ndani ya Ligi ya Wanawake Tanzania huku raundi ya 8 ikiwa ni ya kipekee kwenye upande wa mabao ya jumla kufungwa ambayo ni 16.
Ikumbukwe kwamba raundi ya 7 yalikusanywa jumla ya mabao 12 huku ile raundi ya sita yakikusanywa jumla ya mabao 13. Rekodi hizo katika raundi mbili zote zimevunjwavunjwa raundi ya 8.
Fountain Gate Princess ikiwa nyumbani ilishuhudia ubao ukisoma 0-4 Simba, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Ceasiaa Queens 2-1 Alliance Girls, Uwanja wa Samora, Aman Queens 1-0 Bunda Queens, Uwanja wa Ilulu, Lindi, JKT Queens 6-0 Baobab Queens, Uwanja wa Azam Complex na Yanga Princess 2-0 Geita Gold Queens, Azam Complex.
Ni JKT Queens hawa waliokutana na rungu la kupokwa mechi tano walipata ushindi mkubwa kuliko timu zote raundi ya 8 huku timu moja ikishinda ugenini na nne zilishinda mechi zao za nyumbani.