Kiungo wa Kikosi cha Yanga, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, leo ametarajiwa kuanza mazoezi na wenzake majira ya saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Avic Town baada ya kupona majeraha ya mkono yaliyokuwa yakimkabili.

Sure Boy aliumia mkono kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Februari 2, 2024 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Awali baada ya kuumia, taarifa ya daktari ilionesha kuwa kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili, hivyo tayari amepona na kuungana na wenzake.

Kupona kwake, kunamfanya kiungo huyo kuwa sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaochezwa Februari 17, 2024, ambao Yanga itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here