Kocha Jose Mourinho yupo kwenye mazungumzo na Chama cha soka cha Cameroon kwenda kuinoa timu ya taifa hilo jambo ambalo linaonekana kupiga hatua kubwa
Mourinho anatafuta changamoto mpya baada ya kutimuliwa katika klabu ya AS Roma mnamo Januari 2024, kufuatia mfululizo mbaya wa matokeo ligi kuu Italia .
Endapo mazungumzo yakienda sawa anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ingawa mshahara unatajwa unaweza kuwa kikwazo.