KIMATAIFA

NOVATUS ATAMBULISHWA RASMI UTURUKI

Mchezaji kiraka wa kimataifa wa Tanzania Novatus Dismas Miroshi amejiunga na kutambulishwa rasmi na klabu ya Goztepe Spor Kulubu ya ligi kuu soka nchini Uturuki akitokea Zulte Waregem ya ligi kuu soka nchini Ubelgiji.

Novatus ambaye alianza vizuri msimu uliopita akiwa na Shakhtar Donetsk ya Uturuki alipokuwa kwa mkopo kwenye ligi kuu nchini humo na ligi ya Mabingwa Ulaya hakumaliza vizuri baada ya kukosa nafasi ya kuanza mara kwa mara.

Klabu ya Goztepe aliyojiunga nayo Nova, msimu uliopita ilimaliza nafasi ya 2 kwenye ligi daraja la kwanza Uturuki na kufanikiwa kupanda ligi kuu msimu huu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button