Kocha wa timu ya Taifa la Denmark Kasper Hjulmand, ameweka wazi jinsi ambavyo timu ya Manchester United wameingia nao makubaliano juu ya kumpunguzia dakika za kucheza straika wao Rasmus Hojlund
Hojlund ndiyo kwanza amerejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli katika mchezo dhidi ya Liverpool na licha ya kwamba hakuwapo uwanjani kwa muda mrefu, Denmark imemjumuisha hivyo hivyo kwa ajili ya mechi zao za kirafiki dhidi ya Uswisi na Visiwa vya Faroe.
“Tumekubaliana na Man United kuhusu muda wa kucheza kwa mshambuliaji Hojlund kwenye mechi hizo mbili. Hii kitu ni kizuri kwa upande wetu na upande wao pia.” amesema kocha wa Denmark, Hjulmand