KIMATAIFA

USM ALGER YACHAPWA NIGERIA ‘CAFCC’

Bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika, USM Alger amepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Rivers United kawenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio, Nigeria.

Bao la Augustine Okejepha la dakika ya 10 lilitosha kuitangulizia mguu mmoja kwenye nusu fainali ya michuano hiyo huku ikisikilizia mchezo wa marudiano utakaopigwa Aprili 8, 2024 ugenini Algeria

Rivers United tangu katika hatua ya makundi haijapoteza mchezo wowote wa nyumbani huku USM Alger ikiwa ni mechi ya pili kupoteza kwenye michuano hii.

Hii inakuwa ni mechi ya kwanza kwenye robo fainali na mechi nyingine tatu zitapigwa leo kuanzia saa 2:00 usiku, Stade Malien itaikaribisha Dreams.

Saa 4:00 usiku itapigwa mechi kati ya Abu Salim na RSB Berkane kwenye Uwanja wa Benina Martyrs nchini Libya, wakati Future FC itaialika Zamalek mjini Cairo, Misri.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button