Baada ya kuwasha moto na kuwa mchezaji bora wa michuano ya kombe la Mataifa Amerika (Copa-America) kiungo mshambuliaji na nahodha wa timu ya Taifa ya Colombia James Rodriguez yupo mbioni kurejea kwenye ligi kuu Hispania baada ya klabu ya Rayo Vallecano kumpa ofa ya kujiunga nao kwa msimu mmoja.
Rodriguez ambaye alishindwa kumaliza msimu akiwa na Sao Paulo ya ligi kuu Brazil alikuwa mwiba mkali kwenye Copa-Amerca na kufanikiwa kutoa asisti 6 na kuisaidia timu yake kutinga fainali huku Argentina ikitwaa taji hilo.
Rodriguez anarejea La Liga baada ya awali kuichezea Real Madrid alipowahi kutwaa taji la UEFA Champions League.