Inaelezwa kuwa nyota wa zamani wa Manchester United Mason Greenwood anakaribia kubadilisha taifa atakaloliwakilisha kwenye soka.
Taarifa za ndani kabisa Chama cha Soka nchini Jamaica ‘JFF’ kimeanza mchakato wa kukamilisha swala hilo na tayari wamepeleka maombi FA ya Uingereza kukamilisha jambo hilo.
Timu ya Taifa ya Jamaica maarufu kama Reggae Boyz Kwa sasa wapo chini ya Kocha wa zamani wa Manchester United Steve McClaren.
Nyota huyo amewahi kuitumikia timu ya taifa ya England mchezo mmoja tuu kabla ya kukumbana skendo ya kumnyanyasa mpenzi wake kingono.
Skendo hiyo ilimfanya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Garath Southgate kusema kuwa hatokaa amuite tena nyota huyo kwenye kikosi cha Three Lion.