Kocha wa Simba Abdelhak Benchikha ameondoka nchini leo kulekekea nyumbani kwao Algeria kwa ajili ya kozi ya siku tano kisha atarejea kuendelea na majukumu yake.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema makocha wasaidizi wa timu hiyo watavaa viatu vya kocha huyo kipindi atakapokosekana.
Ahmed ameongeza kuwa kocha huyo atakosekana katika michezo miwili ya timu hiyo dhidi ya Coastal Union Machi 9 na Singida Fountain Gate Fc utakaopigwa katika uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro Machi 12 mwaka huu.
https://youtu.be/jc96t4yYyZk