Simba ina habari njema juu ya beki wake wa kati, Abdulrazack Hamza ambaye alipata majeraha muda mfupi baada ya kujiunga na kambi ya timu ya taifa Taifa Stars’ hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbili dhidi ya DR Congo za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025.
Baada ya matibabu ambayo Hamza ameyapata chini ya uangalizi wa jopo la madaktari wa Simba, beki huyo yupo katika maendeleo mazuri kiafya na leo Jumatatu ataungana na wenzake kikosini kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga, Jumamosi Oktoba 19 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa