KITAIFA
MTIBWA SUGAR 0-2 AZAM FC
FT: Uwanja wa Manungu
Ligi Kuu Bara
Mzunguko wa pili
Mtibwa Sugar 0-2 Azam FC.
Feisal Salum goal dakika ya 20
Gibril Sillah goal dakika ya 65.
Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila inapambana kupata pointi tatu kujinusuru hatari ya kushuka daraja.
Inapambana na Azam FC ambayo inasaka nafasi ya pili kufanikisha malengo ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Ipo wazi kwamba vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 65 kibindoni baada ya kucheza mechi 25 msimu wa 2023/24.
Simba wapo nafasi ya tatu na mchezo wao ujao Mei 9 ni Mzizima Dabi dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.