NYOTA watatu kati ya sita waliotemwa na Simba katika dirisha dogo, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke na Shaaban Idd Chilunda wamepata dili baada ya kunaswa na Mtibwa Sugar na KMC.

Mwanuke na Kapama wametua zao Mtibwa, wakati Chilunda aliyewahi kuwika na Azam FC akisajiliwa KMC ili kuendeleza moto alioshindwa kuuwasha Msimbazi.

Kapama alisema ni kweli amemalizana na Mtibwa kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuvunjiwa mkataba na Simba sasa atakuwa huko kuipambania timu hiyo isishuke daraja.

“Nimemalizana na Mtibwa nitacheza huko kwa miezi sita naamini ni chaguo sahihi baada ya ofa nyingi nilizokuwa nazo naamini nitapambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuiondoa timu hiyo kwenye hatari ya kushuka daraja.” alisema Kapana.

Wakati huohuo rafiki wa karibu wa Mwanuke amefichua kuwa beki huyo amejiunga na Mtibwa kwa mkopo akitokea Simba.

“Mwanuke ametolewa kwa mkopo na Simba ili aweze kuisaidia Mtibwa kukwepa janga la kushuka daraja kutokana na kuwa katika nafasi mbaya,” kilisema chanzo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here