Habari za Yanga
VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wanakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania.
Yanga Aprili 20 2024 imetka kukomba pointi tatu dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi.
Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-1 Simba hivyo ndani ya msimu wa 2023/24 nje ndai Simba kapoteza.
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema wanatambua mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa hivyo wapo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu.
“Ni mchezo ambao unaushindani mkubwa hasa ukizingatia wapinzani wetu sio timu yakubeza kwa kuwa tulikutana nao mzunguko wa kwanza.
“Tupo tayari na wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo wetu hivyo ni suala la kujitokeza kwa wingi mashabiki wetu kushuhudia burudani,”.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mej General Isamuhyo Aprili 23 2024 ambapo Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 58 JKT Tanzania nafasi ya 15 na pointi 22.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here