BAADA ya timu 8 kupata ushindi na kutinga hatua ya robo fainali CRDB Federation Cup tayari kila mmoja katambua atacheza na nani katika msako wa ushindi kuelekea hatua ya nusu fainali.
Ipo wazi kwamba mabingwa watetezi ni Yanga hawa wanatarajiwa kumenyana na Tabora United nyuki wa Tabora katika hatua ya robo fainali.
Matajiri wa Dar, Azam FC wao watakuwa nyumbani kusaka ushindi mbele ya Namungo FC na Coastal Union ya Tanga itakuwa dhidi ya Geita Gold wakati Ihefu wao watamenyana na Mashujaa.
Simba watakuwa mashuhuda wa bingwa mpya kwa mara nyingine tena kwa kuwa wamegotea hatua ya 16 bora walifungashiwa virago na Mashujaa kutoka Kigoma.