Aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Daniel Cadena ameipa mkono wa kwaheri klabu hiyo huku akieleza kuwa ulikuwa ni wakati mzuri kuhudumu ndani ya viunga vya Wekundu hao wa Msimbazi.

“Siku kama ya leo Julai 6, 2023, nilifika nyumbani kwa SIMBA SC na kupokelewa kwa furaha. Leo, Julai 6, 2024, kwa sababu za kitaaluma, ninaondoka mahali hapa ambapo patakuwa nyumba yangu na ambayo nitapapenda daima kama familia yangu.” amesema Cadena kupitia waraka wake wa ‘thank you’ kwa Mnyama.

“Mwaka uliojaa wakati mzuri na usio-mzuri … mwaka ambao nimejifunza mambo mengi na kukutana na watu wa ajabu.”

“Ili nisimsahau mtu yeyote; Ninawashukuru wale wote wanaoipenda klabu na ambao wamekuwa wakifanya kazi kila siku kwa weledi, elimu, na heshima, wakijitolea kila wakati. Kwenu nyote, ASANTENI!!”

“Napenda kuwashukuru watu wote, Rais, Mkurugenzi Mtendaji na bodi ya wakurugenzi walioniwezesha kutetea jezi hii ya SIMBA SPORT CLUB. ASANTE!!”

“Shukrani kwa makipa wangu, SITAWASAHAU, kwa sababu mmeniheshimu na kunithamini kila wakati. Kwangu mimi ninyi ni watoto wangu watano kutoka Tanzania. Nawatakia kila la kheri kwa maisha yako yajayo!!”.

Aidha Cadena raia wa Uhispania amewashukuru mashabiki wa Simba Sc kwa upendo waliomuonyesha kila mara katika kila sehemu ya nchi aliyotembelea.

“Pamoja na wewe, kila kitu kimekuwa rahisi, na asante kwako, nilivumilia hadi mwisho wa msimu. ASANTENI MASHABIKI WA SIMBA!!” amesema Cadena na kuongeza “Kutoka moyoni mwangu naitakia kila la heri Simba Sport Club. Hakika nitarudi!!”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here