Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa la Morocco, Walid Regragui amesema kwamba katika mchezo wao wa leo dhidi ya Taifa Stars wataingia kwa kuiheshimu Tanzania kwani wanaamini hakuna timu ya kuichukulia poa kwenye AFCON hii

“Tutaingia Uwanjani huku tukiiheshimu Tanzania, tumeshuhudia katika michezo ya awali kwa wenzetu wakisumbuliwa na timu zenye hadhi kama ya Tanzania na hii inaizidi kudhihirisha kwamba mashindano haya ni magumu msimu huu. Tunatakiwa kupambana kwasababu kila mmoja anataka kuweka historia yake.” amesema Kocha Walid Regragui

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here