Baada ya mfululizo wa matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu Uingereza 2024-25 Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Manchester United Omar Berrada amesema utawala wa timu hiyo una imani kubwa na kocha mkuu wa timu hiyo Erik Ten Hag ambaye amekuwa akipondwa sana na mashabiki wa timu hiyo.
“Tunafikiri Erik Ten Hag ndiye kocha sahihi kwetu na tunamuunga mkono kikamilifu kwa 100%” alisema Berrada ambaye ni C.E.O wa Manchester United baada ya kipigo cha 3-0 kutoka kwa Liverpool.
Uongozi wa timu hiyo chini ya kampuni ya INEOS iliyo chini ya tajiri wa Uingereza Sir Jim Ractliffe umeendelea kumuunga mkono kocha huyo licha ya kukataliwa na mashabiki kutokana na mbinu zake.