YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi baada ya kucheza mechi nne ambazo ni dakika 360 imekomba ushindi mechi zote za Ligi Kuu Bara.
Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wa taji la ligi walitwaa msimu wa 2023/24 walipomaliza msimu wakiwa na pointi 80 kibindoni baada ya kucheza mechi 30.
Kwa msimu wa 2024/25 baada ya mechi nne safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 8 na ukuta haujaruhusu kufungwa ndani ya uwanja katika mechi za ushindani.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya nne na pointi zake kibindoni ni 12 ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 ilimaliza ikiwa namba moja kwa timu ambazo zilifungwa mabao machache ambayo ni 14.
HIZI HAPA MECHI ZA YANGA
- Kagera Sugar 0-2 Yanga
- Ken Gold 0-1 Yanga
- Yanga 1-0 KMC
- Yanga 4-0 Pamba Jiji.
Mchezo ujao kwa Yanga ni Kariakoo Dabi dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 19 2024 kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu uwanjani.