KIUNGO wa Yanga, Clatous Chama amesema ndoto yake kuvaa medali za ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF), itawezekana akiwa ndani ya klabu yake ya sasa.
Amesema 2020 alipishana na ubingwa huo alipotoka RS Berkane ya Morocco walipotwaa ubingwa huo baada ya kurejea Tanzania kujiunga na Simba.
RS Berkane msimu wa 2020 imefanikiwa kutwaa Ubigwa huo baada ya kuitungua Pyramids FC kutoka Misri kwa 1-0, bao pekee la ushindi la dakika ya 15 limefungwa na mshambuliaji kutoka Burkina Faso Issoufou Dayo.
Chama amesema ndoto kwenye michuano ya CAF ni kuchukuwa ubingwa wa klabu bingwa Afrika ukiacha kuwa mfungaji bora wa Afrika, ndoto yake kubwa ni kuona anabeba kombe hilo na kuvaa medali.
“Ubingwa Afrika ndio ndoto yangu kubwa niliukosa RS Berkane, nikiwa Yanga inawekezaka kwa sababu tunavyona sasa hivi timu iko vizuri sana, natamani sana timu ifike fainali na tutimeze hiyo ndoto kama timu, kitu kikubwa kushinda ligi ya mabingwa,” amesema Chama.