Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize anasema ingawa mguu wake wa asili anaoutegemea katika soka ni wa kulia, lakini mguu wa kushoto ndiyo una nguvu zaidi ya kupiga mashuti, kukokota mpira na kutoa pasi kuliko wa kulia.
“Mimi mguu wangu ni wa kulia, lakini mguu wa kushoto unakuwa na nguvu zaidi kwa kutoa pasi na kukokota mpira na uko vizuri kufanya hivyo kuliko wa kulia na hiki kitu hakikuja kwa bahati mbaya, nimejifunza na nimefanya hivyo kwa kuwaangalia wachezaji wa nje akiwamo Cristiano Ronaldo, yule jamaa mguu wake wa kulia, lakini akipiga kushoto kama kulia.
Kwa sasa ukitaka kuwa mchezaji bora ni lazima uwe una uwezo wa kutumia miguu yote miwili, hata kama haitokuwa na nguvu sawa, lakini ikaribiane,” aliongeza mchezaji huyo.