Kiungo wa kati wa Croatia, Luka Modric, amemtaja Bernardo Silva kama mchezaji mwingine wa Ureno anayempenda mbali na Cristiano Ronaldo.
Nahodha huyo wa Real Madrid ameyasema hayo kabla ya mechi ya Kundi A ya Ligi ya Mataifa ya Croatia dhidi ya Ureno itayopigwa usiku wa leo Alhamisi mjini Lisbon.
“Kwenye kikosi cha Ureno, kando na Cristiano Ronaldo, Bernardo Silva ndiye mchezaji mwingine ninayempenda” alisema Modric.