KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameweka wazi anahitaji kutengeneza muunganiko wa safu ya ushambuliaji ambao utamnufaisha kwa kupata idadi ya mabao mengi katika michezo iliyopo mbele yao kwa msimu wa 2024-2025.
Amesema mechi ya kirafiki ya kimataifa, dhidi ya Al Hilal imemsaidia kuona kile anachokihutaji hasa kuona muunganiko wa kila nafasi na mchezaji waliopo ndani ya kikosi chake.
Fadlu ametumia mchezo huo wa kirafiki kuandaa kikosi cha Simba kuelekea mechi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya ambao wataanzania ugenini.
Fadlu amesema amepata somo alilohitaji kupata kupitia mchezo huo kwa kumpa nafasi kila mchezaji kuweza kuonyesha uwezo wake na hakuangalia matokeo ya dakika 90.
Amesema bora wamejifunza makosa kama kocha alikuwa akiwaonya wachezaji wake wakati wa mapumziko na kile alichokisema kilifanyika kutoka kwa mchezo huo ulikuwa uzoefu na bora wamepata somo kabla ya kwenda Libya dhidi ya Al Ahly Tripoli.
“Nimeweza kuwapa nafasi hasa safu ya ushambuliaji ilikuwa na washambuliaji wanne ulikuwa ni mchezo kwa kwanza kucheza Awesu (Awesu) akucheza na Chasambi (Ladack ) akucheza na Kibu (Dennis) ambaye hakuwa kwenye Pre Season.
Ateba (Leonel) ambaye yuko katika wiki ya tatu tu ya maandalizi ya msimu mpya kwa hivyo ni kawaida kwamba huna muunganisho huo na safu mpya ya ushambuliaji kwa sababu Valentino (Mashaka) amefunguka mechi mbili na Mukwala (Steven) amefunga pia,” amesema Kocha huyo.
Kuhusu Joshua Mutale amesema anarudi na kuonyesha kwamba anaweza kucheza kwa dakika nyingi katika mchezo ujao bila majeruhi na ndivyo anafanya.
“Nahitaji kuona kikosi kipo imara kila mchezaji anakuwa na kiwango bora ikiwa mchezaji anacheza sio kusema pumzika kwa sababu kuna mmoja anasubiri kuchukua nafasi zao.
Nimefanikiwa na kwa kweli nimefurahishwa na nilichokiona hasa kipindi cha kwanza na masomo ya kipindi cha pili ni ya ajabu kwangu kama kocha kuweza kufanya uchambuzi ili kuweza kupitia na timu kuongeza kitu kabla ya kwenda Libya, “ amesema Fadlu.
Naye kocha wa Al Hilal, Florent Ibenge amesema ulikuwa mchezo mzuri walikuja kutafuta ushindi lakini wamepata sare na kupata maandalizi mazuri.
“Hatukucheza vizuri kipindi cha kwanza kwa sababu tuliamua kucheza nyuma, hii ni kutokana na kuwakosa wachezaji wetu ambao wapo kwenye timu ya Taifa,”
Tuliamua kuwapa mpira wapinzani katika kipindi cha kwanza na tukaruhusu bao kutokana na makosa binafsi, lakini hatukukata tamaa,” amesema Ibenge.
Ameongeza kuwa aliongea na wachezaji wake baada ya kipindi cha kwanza kufanyia kazi makosa na kuwa bora kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha.
“Mwamuzi alitupa kadi nyekundu ambayo haikuwa ya haki (Unjustified red card), kitu ambacho kilituongezea ugumu lakini tuliweza kuhimili tukasawazisha bao na huenda tungepata hata bao la ushindi kwa sababu tulitengeneza nafasi za wazi,” amesema kocha huyo wa Al Hilal.