KUELEKEA katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Vital’O dhidi ya Yanga uongozi wa Yanga umebainisha kuwa watawaonyesha kwa vitendo wapinzani hao.
Ni Agosti 17 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni hatua ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa tayari huku wapinzani wao wakiwa na tambo ambazo zitawapa kile wanachokitaka.
“Sisi Wanayanga tunataka kuwaonyesha Vital’O kwa vitendo tuwaambie kuwa kwa sasa acha wacheze kwa maneno sisi tutafanya kwa vitendo, wachezaji wote wapo fiti kwa mchezo huo.
“Ni mchezo mkubwa na tunakwenda kwenye mchezo tukiwa tayari, tambo ambazo wanazifanya sisi tunaandika, sasa hivi acha wazungumze maneno yao tutakutana nao Uwanja wa Azam Complex. “
Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Clatous Chama, Aboutwalib Mshery, Djigui Diarra, Sure Boy, Aziz Ki, Farid Mussa, Maxi Nzengeli, Pacome.