Manara na Ahmed Ally

Katika muendelezo wa tambo mbali mbali za Simba na Yanga pindi ukiotewa pale ambapo pana mshono hakika nawe lazima ukajipange kuja kurudisha mashambilizi.

Picha ya zamani ya Ahmed Ally akiwa ameshika kombe la Yanga sasa imetumiwa vizuri na Manara kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Ahmed naye pia ni mpenzi wa Yanga japo tupo Simba kwenye kujitafuta

Ahmed Ally Picha ya zamani akiwa na kombe la Yanga
Ahmed Ally Picha ya zamani akiwa amekumbatia kombe la Yanga

Manara ameandika “Nakiri kwamba hata mimi wakati najitafuta, niliibukia kuwa Mfuasi feki wa Madunduka, na ilifika mahali nikawa nawacharura mno Yanga hadi mimi mwenyewe ilikuwa inanikera, lakini ndio kujitafuta huko, ningefanyaje ndugu zangu? Na bila kufanya hivyo GSM wangenionaje ? Ile Siku waliyoniambia rudi home sasa, ooohh ilikuwa siku kubwa sana kwangu, SITASAHAU

Basi bhana Wakulungwa, ndio story ya huyu kijana mkazi wa Tambuka Reli, kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu,ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu, huyu anaumwa na Yanga yake, hali hata Chakula siku Wananchi wakiwa wanacheza, Kigosi @raythegreatest na @jimmymafufu waliwahi kuniambia walikuwa wanampa hadi hirizi kuvaa,siku ya mechi ya Yanga 😝

Miaka ya nyuma ilikuwa kila asubuhi anaenda Jangwani kubusu na kupiga picha na Makombe yetu, na akifika tu anaamkia, Shkamoo Makombe😜 na Wazee wetu pale klabuni walikuwa wanampenda kwa ule usafi wake wa kusafisha kila siku Makombe yetu, hadi Jiki alikuwa anayaoshea.🤪

Kwa hiyo msameheni Wanayanga, anajitafuta tu,ni kijana wetu mzuri na ana msaada mkubwa kwetu, Mtu wa maana sana na ni familia kabisa, Soon Mtanielewa Wananchi”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here