ken gold yapanda ligi kuu

Baada ya kusota kwa misimu mitatu mfululizo bila mafanikio, hatimaye Ken Gold imepanda Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FGA Talents.

Mabao pekee na ya kihistoria yaliyoipandisha timu hiyo yamefungwa na Mishamo Michael na Robert Mackidala na kuifanya Ken Gold ya wilayani Chunya Mkoani Mbeya kufikisha pointi 67 na kujihakikishia nafasi ya Ligi Kuu msimu ujao.

Mchezo huo ambao umepigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Ken Gold ilihitaji ushindi tu ili kujihakikishia nafasi hiyo na haikufanya makosa na kufikia malengo yake.

Pointi 67 za timu hiyo zinaweza kufikiwa na Pamba Jiji tu iwapo atashinda mechi ya mwisho dhidi ya Mbuni baada ya mchezo wa jana kutakata kwa mabao 2-1 dhidi ya TMA na hivyo timu hizo zitapanda zote moja kwa moja.

Hata hivyo, kitendo cha Biashara United kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Pan African, yanaipa nafasi kubwa Pamba Jiji kutafuta japo sare katika mchezo ujao ili kujihakikishia ndoto yake ya zaidi ya miaka 20, bila Ligi Kuu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here