KITAIFA

AHMED ALLY: KAMA TUSIPOFUZU MAKUNDI UBAYA UBWELA UTATURUDIA

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya, itakayochezwa ugenini Septemba 15, 2024, itakuwa ngumu.

Hata hivyo, amesema wamejipanga vyema ili kupata ushindi utakaowaweka katika nafasi nzuri kwa mechi ya marudiano.

Pia amesisitiza, itakuwa aibu kubwa endapo timu hiyo itashindwa kufuzu makundi, na kwamba kauli mbiu ya ‘Ubaya Ubwela‘ itawarudia kutokana na matarajio makubwa waliyojiwekea ya kufanikiwa 2024/25.

“Katika mechi tunayokwenda kucheza Libya, ni mechi ya wachezaji na benchi la ufundi, wao ndio wana jukumu la kutuvusha kuingia hatua ya makundi”

“Itakuwa ni fedheha kinouma nouma, itakuwa ni aibu kubwa na ubaya ubwela utatrudia kama tusipoweza kuingia kwenye hatua ya makundi, wanasimba tutaonea aibu wenyewe kwa wenyewe kwa ile aibu ya kushindwa kutinga hatua ya makundi.” Ahmed Ally

Mchezo wa kwanza hatua ya kwanza ya kombe la shirikisho kati ya Al Ahli Tripoli itapigwa, siku ya Jumapili Septemba 15, huko nchini Libya.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button