Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mnamo August 09,2024 imetupilia mbali mwenendo mzima wa maombi yaliyofunguliwa na Juma Magoma na wenzake ya kutaka kuundoa uongozi wa Club ya Yanga madarakani na pia kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa katika hukumu iliyowapa ushindi Wazee hao.
Pamoja na kutupilia mbali maombi yao, Mahakama hiyo imeamuru Magoma, Geofrey Mwaipopo na Abeid Mohamed Abeid walipe kwa Muombaji ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya Club ya Yanga, gharama zote za uendeshaji wa shauri hilo.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, wakati akitoa uamuzi wa marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022 yaliyoombwa na Bodi hiyo kwa madai kuwa Wazee hao hawakuwa na sifa ya kufungua shauri.