Sakata la Fiston Mayele limemuibua mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa ambaye amesema kama ni kutupiwa jini basi Fei Toto angekuwa chizi, majini ya hapahapa na yanamuona kuliko majini ya kusafiri.

“Kuna kipindi nilihamia team nyingine kutoka yanga nikakuta kule mashabiki wachache nishazoea shangwe kufunga kukawa shida nikasema ndio nimeisha au Ikn sikuwaza majini” ameandika Ngassa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“Kuna wachezaji wakitoka Simba, Yanga, Azam kufunga ni ngumu wanaenda team Mashabiki wapo 30 mpinzani haogopi chochote, uwezo wako ndio watakiwa uwaonyeshe. Sasa umeondoka ktk team umeuzwa watu wamepiga pesa wamefurahi unakuja umetupiwa jini.

“Basi Fei Toto angekuwa chizi majini ya kusafiri na majini ya hapa hapa yanamuona. Hahaha team ni kubwa kuliko mtu yoyote hii ni story fupi wachezaji. Kuna maisha baada ya soccer tuishi vizuri na shule tulizo pita kesho tutasomesha watt wetu kwa Ada ndogo” — Ngassa

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here